Ni ipi hukumu ya kumuomba du´aa maiti?

Swali: Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema katika Majmuu´-ul-Fataawaa kwamba kumuomba maiti akuombee du´aa kwa Allaah ni kitendo cha Bid´ah ambacho hakikufanywa na Salaf na haizingatiwi kuwa ni kufuru wala shirki bali ni katika Bid´ah. Je, nukuu hii kutoka kwake ni sahihi?

Jibu: Midhali umesema yanapatikana katika Majmuu´-ul-Fataawaa yote yanayopatikana humo – Allaah akitaka – ni sahihi na yenye kutegemewa.

Lakini hata hivyo hakusema kuwa inajuzu kuomba du´aa kutoka kwa maiti. Badala yake amesema kuwa ni Bid´ah na kuwa haijuzu. Kusema kwamba ni shirki au sio shirki kunahitajia ufafanuzi juu ya hali ya mwombaji na muulizaji huyu.

Maiti haombwi kitu kwa sababu matendo yake yamekatika. Du´aa ni matendo. Unamuomba maiti kitu asichokiweza. Maiti hawezi kuomba na wala hawezi kukutakia msamaha. Madhambi yake mwenyewe hawezi kujiombea msamaha kwayo. Ni vipi basi ataweza kukuombea du´aa na msamaha? Yeye ni mwenye haja ya kukhafifishiwa adhabu ya kaburi na wala hawezi kumuomba Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2104
  • Imechapishwa: 28/06/2020