Ni ipi hukumu ya kukusanya du´aa mbili za kufungulia swalah katika swalah moja?

Swali: Ni ipi hukumu ya kukusanya du´aa mbili za kufungulia swalah katika swalah moja?

Jibu: Sunnah ni kusoma du´aa moja ya kufungulia swalah. Haikutufikia kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikusanya kati ya du´aa mbili za kufungulia swalah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 100-101
  • Imechapishwa: 07/07/2018