Wudhuu´ unasihi katika chombo cha dhahabu na fedha?

Swali: Je, wudhuu´ unasihi katika chombo cha dhahabu na fedha?

Swali: Haijuzu kutumia vyombo vya dhahabu na vya fedha. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuvitumia. Lakini hata hivyo kutawadhia ndani  yavyo kunasihi pamoja na kuwa ni haramu. Kwa sababu lengo limefikiwa. Baadhi ya wanachuoni wamekataza hilo – na hayo ndio maoni ya mwandishi. Kutumia vyombo vya dhahabu na vya fedha haviruhusiwi kwa sababu ni kama vyombo vilivyoporwa. Havisihi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kufanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu basi atarudishiwa mwenyewe.”

Wale ambao wanaonelea kuwa umesihi wamesema kwamba lengo ni twahara na tayari imekwishapatikana kwa maji na wanaonelea kuwa dhambi haizuii. Ni kama mtu akijitupa kwenye bwawa na akatawadha pasi na kupewa idhini na mwenye nayo, akafanya Tayammum kwenye udongo wa ardhi ya watu pasi na kupata idhini yao na mfano wa hayo. Lengo ni ile twahara na tayari imekwishapatikana. Kupata kwake dhambi kwa kule kutumia kitu ambacho hafai kwake kukitumia hakuzuii kusihi kwa wudhuu´. Kilichokatazwa ni kitendo kitendo cha kupora na dhuluma na sio wudhuu´. Lakini lililo salama zaidi kwa muumini ni yeye arudi kutawadha upya na ajiweke mbali na mambo ambayo wanachuoni wametofautiana. Ahakikishe hatawadhi isipokuwa kwa kutumia maji yaliyoruhusiwa. Kwa ajili hiyo ndio maana mwandishi amekata ya kwamba kuruhusiwa kwa maji ni sharti ya kusihi kwa swalah kwa kutumia msingi unaosema:

“Yale niliyokukatazeni basi jiepusheni nayo… “

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 66