Ni ipi hukumu ya kukiswalia kipomoko kilichodondoka?

Swali: Je, ni lazima kukiswalia na kukitolea swadaqah kipomoko kikipitikiwa na miezi miwili au chini ya hapo?

Jibu: Itategemea. Ikiwa kipomoko hiki kimechapitisha siku arobaini na kimeshapuliziwa roho, hiki kikiporomoka basi kinaoshwa, kinaswaliwa, kinapewa jina na kufanyiwa ´Aqiyqah. Kufanya hivo ndio bora. Hivo ndivo wanavosema wanachuoni. Lakini ikiwa ni kabla ya mambo hayo hakioshwi wala hakiswaliwi mpaka pale kitakapoumbwa na kupuliziwa roho. Kukiporomoka kinyama au damu basi haizingatiwi ni chochote na wala hakitooshwa wala kuswaliwa. Kuoshwa, kikaswaliwa na kupewa jina pale ambapo kitaporomoka baada ya miezi arobaini na tayari kimeshapuliziwa roho.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4556/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D9%86%D9%8A%D9%86-%D8%A7%D9%84%D8%B3%D9%82%D8%B7
  • Imechapishwa: 14/11/2020