Swali: Ni ipi hukumu ya kujenga juu ya makaburi?
Jibu: Kujenga juu ya makaburi ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hilo kutokana na kule kuwatukuza wafu na sababu nyingine hiyo ni njia ya kuabudiwa makaburi haya na kufanywa ni washirika pamoja na Allaah. Hivo ndivo ilivyo hali ya majengo mengi yaliyojengewa juu makaburi. Hatimaye watu wakaanza kuwaomba wafu wale na kumshirikisha Allaah (Ta´ala). Kuwaomba wafu na kuwataka msaada ili kuondoa matatizo ni shirki kubwa na kuritadi nje ya Uislamu.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/212)
- Imechapishwa: 25/05/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Ni ipi hukumu ya kuyajengea makaburi?
Swali: Ni ipi hukumu ya kuyajegea makaburi? Jibu: Kuyajengea makaburi ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza hilo kwa vile ndani yake kunapatikana kuwaadhimisha wafu. Sababu nyingine ni kwa vile ni njia inayopelekea makaburi haya kuabudiwa na kufanywa mungu pamoja na Allaah. Hivyo ndivyo ilivyo hali ya majengo…
In "Shirki na aina zake"
24. Ni ipi hukumu ya kulijengea kaburi?
Swali: Ni ipi hukumu ya kulijengea kaburi? Ni ipi hukumu endapo kile kilichojengwa ni msikiti? Jibu: Kulijengea kaburi ni jambo la haramu. Ni mamoja kile kilichojengwa ni msikiti, kuba au jengo. Haijuzu kufanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: ”Allaah awalaani mayahudi na manaswara. Wameyafanya makaburi ya Mitume…
In "at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur - Ibn Baaz"
Ni ipi hukumu ya wale wanaoyaomba wafu ndani ya makaburi?
Swali 2: Yale yanayofanywa na baadhi ya wajinga pambizoni na makaburi katika kuwaomba wafu, kuwataka msaada, kuwataka uombezi, kuwaomba nusura dhidi ya maadui au kuwaomba uokozi. Ni ipi hukumu yake? Kwa sababu mambo haya yanafanyika katika miji mingi. Jibu: Kwa jina la Allaah na himdi zote njema ni stahiki ya…
In "Akhtwaau fiyl-´Aqiydah - Ibn Baaz"