Ni ipi hukumu ya kuiazimia Qur-aan kutokana na tuzo za leo?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuazimia miujiza ya Qur-aan kwenye tuzo za leo?

Jibu: Qur-aan ni miujiza bila ya shaka:

قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا

“Sema: “Ikiwa watajumuika wanadamu na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan; hawatoweza kuleta mfano wake, japokuwa watasaidiana wao kwa wao.” (17:88)

Ni miujiza bila ya shaka. Ni miujiza katika mpangilio wake. Ni miujiza katika usulubu wake. Ni miujiza katika hukumu zake. Ni miujiza katika kuyaelezea mambo yaliyofichikana. Ni miujiza katika mambo ya Shari´ah. Ni miujiza kwa njia zote, hili halina shaka.

Hata hivyo haijuzu kuazimia kuwa uvumbuzi wa leo, tiba na mengineyo yametajwa katika Qur-aan. Mtu anaweza kusema inawezekana yaliyotajwa yako katika Aayah au miujiza fulani pasi na kuazimia. Haifai kuazimia na kuifasiri Qur-aan kutokana na kazi za wanaadamu pasi na dalili ya hilo. Qur-aan haifasiriwi isipokuwa kwa Qur-aan, mapokezi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), tafsiri za Maswahabah, tafsiri za Taabi´uun na kwa lugha ya kiarabu. Namna hii ndivyo Qur-aan inavyofasiriwa. Haijuzu kuifasiri Qur-aan kwa njia nyingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-09.mp3
  • Imechapishwa: 08/06/2020