Ni ipi hukumu ya kufunika jeneza la mwanamke kwa nguo wakati wa mazishi?

Swali: Baadhi ya watu pindi jeneza la mwanamke linapoteremshwa kwenye mwanandani wanamfunika na kitambaa. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni jambo lililofanywa na Salaf na wakalipendekeza wanachuoni (Rahimahumu Allaah). Wanachomaanisha ni kuwa nguo inamsitiri vizuri zaidi na kuna khatari akaonekana pindi anaposhushwa kwenye mwanandani. Huku kwetu ´Unayzah watu wanamshusha mwanamke kwenye nguo waliyomfunika nayo. Kisha wanaondosha nguo hii kidogo kidogo kila ambavyo wanamfukia kwa kokoto. Kwa njia hiyo anasitirika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/174)
  • Imechapishwa: 25/08/2021