Swali: Ni ipi hukumu kwa mwanaume kuvaa nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu pasi na kukusudia kiburi?
Jibu: Kuvaa nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu ni jambo la haramu na halijuzu. Ikiwa mtu anavaa kwa kiburi basi dhambi inakuwa kubwa zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kile chenye kuvuka kongo mbili za miguu katika kikoi ni Motoni.”
Hakushurutisha jambo la kuvaa kwa kiburi.
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Watu aina tatu Allaah hatowatazama siku ya Qiyaamah, hatowatakasa na watakuwa na adhabu kali: mwanaume mwenye kuburuta kikoi chake, mwenye kufanya masimango kwa kile alichokitoa na yule mwenye kuuza bidhaa yake kwa kiapo cha uongo.”
Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Tahadhari kutokamana na nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu. Kwani hakika ni katika kiburi.”
Haijuzu kabisa nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu. Lakini mtu akivaa kwa kiburi dhambi zake zinakuwa khatari zaidi.
Lakini mtu nguo yake ikimshinda kwa bahati mbaya na ikamteremka bila ya kukusudia kiburi, bali ni jambo ambalo humtokea baadhi ya nyakati ni jambo linalosamehewa. Hayo yalikuwa yakimpitikia [Abu Bakr] as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomwambia kwamba yeye havai kwa kiburi. Hapo ilikuwa wakati alipomwambia kwamba kikoi chake kinamteremka pamoja na kwamba anajitahidi kukipandisha. Kwa hiyo mtu akipandisha nguo yake lakini hata hivyo baadhi ya nyakati ikamteremka lakini pamoja na hivyo akijitahidi kuipandisha tena ili asiburute hakuna dhambi juu yake. Lakini mtu kukusudia kuiteremsha nguo yake ndio dhambi.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2826/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B3%D8%A8%D8%A7%D9%84-%D9%85%D9%86-%D8%BA%D9%8A%D8%B1-%D9%82%D8%B5%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AE%D9%8A%D9%84%D8%A9
- Imechapishwa: 24/01/2020
Swali: Ni ipi hukumu kwa mwanaume kuvaa nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu pasi na kukusudia kiburi?
Jibu: Kuvaa nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu ni jambo la haramu na halijuzu. Ikiwa mtu anavaa kwa kiburi basi dhambi inakuwa kubwa zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kile chenye kuvuka kongo mbili za miguu katika kikoi ni Motoni.”
Hakushurutisha jambo la kuvaa kwa kiburi.
Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Watu aina tatu Allaah hatowatazama siku ya Qiyaamah, hatowatakasa na watakuwa na adhabu kali: mwanaume mwenye kuburuta kikoi chake, mwenye kufanya masimango kwa kile alichokitoa na yule mwenye kuuza bidhaa yake kwa kiapo cha uongo.”
Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Tahadhari kutokamana na nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu. Kwani hakika ni katika kiburi.”
Haijuzu kabisa nguo yenye kuvuka kongo mbili za miguu. Lakini mtu akivaa kwa kiburi dhambi zake zinakuwa khatari zaidi.
Lakini mtu nguo yake ikimshinda kwa bahati mbaya na ikamteremka bila ya kukusudia kiburi, bali ni jambo ambalo humtokea baadhi ya nyakati ni jambo linalosamehewa. Hayo yalikuwa yakimpitikia [Abu Bakr] as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomwambia kwamba yeye havai kwa kiburi. Hapo ilikuwa wakati alipomwambia kwamba kikoi chake kinamteremka pamoja na kwamba anajitahidi kukipandisha. Kwa hiyo mtu akipandisha nguo yake lakini hata hivyo baadhi ya nyakati ikamteremka lakini pamoja na hivyo akijitahidi kuipandisha tena ili asiburute hakuna dhambi juu yake. Lakini mtu kukusudia kuiteremsha nguo yake ndio dhambi.
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2826/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B3%D8%A8%D8%A7%D9%84-%D9%85%D9%86-%D8%BA%D9%8A%D8%B1-%D9%82%D8%B5%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AE%D9%8A%D9%84%D8%A9
Imechapishwa: 24/01/2020
https://firqatunnajia.com/ni-ipi-hukumu-kwa-mwanaume-kuvaa-nguo-yenye-kuvuka-kongo-mbili-za-miguu-pasi-na-kukusudia-kiburi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)