Ni Bid´ah Kuwachinjia Udhhiyah wafu?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuwachinjia Udhhiyah maiti kwa vile baadhi ya watu wanasema kuwa kuwachinjia maiti Udhhiyah ni Bid´ah na kwamba ni kwa ajili ya waliohai tu. Tunaomba mwongozo kwa jambo hilo.

Jibu: Udhhiyah ni Sunnah kwa waliohai na maiti. Aliyesema kuwa ni Bid´ah amekosea. Maoni ya sawa ni kwamba ni Sunnah kwa waliohai na maiti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichinja kondoo wawili; mmoja wao kwa ajili Muhammad na familia yake wakiwemo waliokwishakufa kama wasichana zake, na kondoo mwingine alikuwa kwa ajili ya wale wenye kumpwekesha Allaah katika ummah wa Muhammad wakiwemo waliohai na waliokwishakufa. Kumchinjia maiti ni kujikurubisha na kumtii Allaah kama anavofanya aliyehai. Kwa hiyo mtu akiwachinjia wazazi wake waliokwishakufa, ndugu yake au mke wake aliyekwishakufa ni kujikurubisha na kumtii Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/17162/هل-الاضحية-عن-الميت-بدعة
  • Imechapishwa: 13/06/2024