Nguo ya juu imemdondoka akiswali

Swali: Bwana mmoja imemdondoka Ihraam yake ambapo sehemu yake ya juu ikaonekana wakati alipokuwa amesimama na kuswali. Je, swalah yake ni sahihi?

Jibu: Mwanaume ndani ya Ihraam huvaa shuka ya juu na shuka ya chini. Hakuna vibaya shuka ya juu ya mtu ikimdondoka wakati yuko anaswali. Kwa sababu inafaa kwa mwanaume kuswali na shuka ya chini pasi na shuka ya chini ingawa bora ni yeye kufunika mwili mzima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiswali mmoja wenu ndani ya nguo moja pasi na kuwa na chochote juu ya bega lake.”[1]

[1] al-Bukhaariy (359) na Muslim (516).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/292)
  • Imechapishwa: 17/05/2026