Kukisia thamani ya bidhaa za biashara

Swali: Pengine isiwezekane, au ikawa vigumu, kwa mfanyabiashara kuhesabu thamani ya bidhaa zake. Je, anaweza kukisia?

Jibu: Haijuzu kukisia. Inafaa kukisia peke yake juu ya mavuno na, baadhi ya wanazuoni, wamejumuisha pia nafaka yake. Haiwezekani juu ya pesa kukisia kwa sababu zinatofautiana. Mtu anapaswa kufanya akiwezacho na achukue tahadhari. Kwa mfano akihesabu kuwa bidhaa alizonazo zinafikia thamani ya 120, basi atoe zakaah ya 120 ili kuitakasa dhimma yake.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/232)
  • Imechapishwa: 17/05/2026