Nguo nzuri kabisa siku ya ´iyd

Katika siku hii iliyobarikiwa imewekwa katika Shari´ah kujipamba na kuvaa nguo yako ilio nzuri kabisa. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“´Umar bin al-Khattwaab aliona nguo ya hariri karibu na mlango wa msikiti akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Unaonaje ukiinunua na kuivaa mbele za watu siku ya ijumaa na wakati wajumbe wanapokujilia.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Hakika si vyengine hakuna wanaovaa hiyo isipokuwa ni wale wasiokuwa na fungu huko Aakhirah.” Kisha baadaye Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akapata nguo hizo akampa vazi moja ´Umar ambaye alisema: “Ee Mtume wa Allaah! Umeinipa nguo kama hiyo baada ya kusema juu yake uliyoyasema.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mimi sijakupa nayo ili uivae.” Hivyo ´Umar akampa nayo ndugu yake mshirikina Makkah.”[1]

[1] Muslim (2068).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 10
  • Imechapishwa: 29/03/2025