Nguo chini ya macho ya miguu bila ya majivuno na kiburi

Swali: Kuna mtu anayevaa nguo inayovuka vifundo vya miguu lakini hafanyi hivo kwa majivuno na kiburi. Je, anapata dhambi?

Jibu: Ndio, unapata dhambi ikiwa nguo au suruwali yako inashuka chini ya kongo mbili za miguu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kile kikoi kilicho chini ya mafundo mawili ya miguu kiko ndani ya Moto.”[1]

Hakufungamanishia kitendo hicho na kiburi.

[1] al-Bukhaariy (5787).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/306)
  • Imechapishwa: 10/05/2026