Swali: Hakika unajua dhambi zinazopatikana katika harusi za leo kama mavazi, nyimbo na kujifananisha na makafiri. Mtu afanye nini ikiwa wazazi wawili wanataka niende nao harusini? Unawanasihi nini vijana wenye dini wanaohudhuria harusi kama hizi na kuchafua sura ya watu wa dini?

Jibu: Ni wajibu kwa wanafunzi wawanasihi na kuwaelekeza watu na wawakataze israfu, ubadhirifu na maasi. Ni wajibu wetu kwa waislamu wote kwa jumla na khaswa ndugu zenu.

Ikiwa unajua kuwa sherehe ina maovu na si wewe wala baba yako nyote wawili hamuwezi kuyaondosha, mwambie kuwa haijuzu kwenda huko. Na aking´ang´ania mwambie kuwa huwezi kumfuata, kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.” al-Bukhaariy (7258) na Muslim (1840).

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖوَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 29/05/2018