Ndoa na ushahidi kwa aliye ndani ya Ihraam

Swali: Je, inajuzu kwa aliye ndani ya Ihraam kufunga ndoa?

Jibu: Hapana, Muhrim haoi wala haolewi. Hivo ndivo imekuja katika Hadiyth Swahiyh:

“Muhrim haoi, haolewi wala hachumbii pia.”

Haifai kwake kuchumbia mwanamke pia muda wa kuwa yuko ndani ya Ihraam.

Swali: Vipi kuhusu Muhrim kutoa ushahidi ndani ya Ihraam?

Jibu: Sijui ubaya wowote wa hilo, kwa sababu sio mwenye kuoa wala kuolewa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24217/حكم-الزواج-والخطبة-لمن-كان-محرما
  • Imechapishwa: 13/09/2024