Swali: Ni ipi nasaha yako kwa yule ambaye ndoa inamzuia kutafuta elimu?
Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hakuweka ndoa ili ikuzuie na matendo mazuri, kutafuta elimu na kulingania katika dini ya Allaah. Baadhi ya watu wanapooa ndoa inawazuia na matendo mazuri mengi. Hii sio sababu ambayo Allaah ameweka ndoa kwa ajili yake. Ameiweka ili wewe na mke wako mzidishe kufanya matendo mazuri, kufanya Da´wah, du´aa, ´ibaadah na kutafuta elimu. Ndoa ni neema. Mtu anapopata neema mpya basi amshukuru Allaah kwayo. Lakini ikiwa unarudi nyuma kila wakati unapopata neema maana yake ni kwamba humshukuru. Allaah amesema:
لَئِن شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ ۖ وَلَئِن كَفَرْتُمْ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٌ
“Mkishukuru, bila shaka Nitakuzidishieni na mkikufuru, basi hakika adhabu Yangu ni kali.” (14:07)
Izungumzishe nafsi yako ya kwamba kila wakati kunapokuja neema mpya basi majukumu na shukurani vinazidi. Hutakiwi kurudi nyuma.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=2697
- Imechapishwa: 20/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)