Ndoa baada ya kujua kuwa msichana alikuwa kishaposwa na mwengine

Swali: Vipi hali ya ndoa endapo mtu atachumbia juu ya posa ya nduguye?

Jibu: Udhahiri ni kwamba ndoa inasihi lakini yule mposaji wa pili anapata dhambi. Kwa sababu makatazo ya kuposa hayahusiani na ile ndoa.

Swali: Hata kama hawakutangaza mahari?

Jibu: Mahari yanaweza kuja baadaye. Kama hakukutajwa mahari atapewa mahari ya wanawake mfano wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23844/حكم-زواج-من-خطب-على-خطبة-اخيه
  • Imechapishwa: 17/05/2024