Ndio Maana Khawaarij Wanaudhuru Uislamu Na Waislamu

Imaam al-Aajurriy (aliyefariki 360 H) amesema:

“[Khawaarij] wanatoka katika Dini kama jinsi mshale unavotoka kwenye upinde wake. Wanasoma [sana] Qur-aan. Mtazidharau Swalah zenu mkizilinganisha na zao, Swawm zenu mkizilinganisha na zao na kisomo chenu mkikilinganisha na chao.”

Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kupitia kwa Allaah. Pamoja na yote haya hayavukii koo zao na isitoshe wanatoka katika Uislamu kama jinsi mshale unavotoka kwenye upinde wake. Tunamuomba Allaah afya. Hii ni balaa. Katika kila zama wataudhuru Uislamu na Waislamu. Kwa ajili hii ndio maana wao ndio shari ya viumbe na ni mijibwa ya Motoni na tunaomba kinga kwa Allaah. Hata kama watasoma Qur-aan, wakasimama visimamo vya usiku, wakafunga mchana na mengi zaidi ya hayo, wao ni mijibwa ya Motoni na shari ya viumbe. Mbora katika wauaji ni yule mwenye kuwaua. Wao ndio wauliwaji wabaya zaidi chini ya mbingu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/159)
  • Imechapishwa: 19/05/2015