Ndio maana ikawa sio wajibu kuzibadilisha rangi mvi

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Badilisha mvi hizi na jiepushe na rangi nyeupe.”[1]

Je, amri hii inafahamisha kuwa ni wajibu?

Jibu: Hapana. Kwa sababu wako Maswahabah ambao hawakuzibadilisha mvi – waliziacha nyeupe. Kwa hiyo kuzibadilisha rangi mvi inapendeza na sio wajibu. Wanazuoni wengi, akiwemo Shaykh Ibn Ibraahiym, Shaykh ´Abdul-Latwiyf bin Ibraahiym, Shaykh ´Umar bin Hasan na Shaykh as-Sa´diy, ndevu zao zilikuwa nyeupe na hawakuzibadilisha rangi. Kwa hiyo ikafahamisha kuwa kuzibadilisha rangi mvi inapendeza na sio wajibu.

[1] Ibn Hibbaan (5471).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (44)
  • Imechapishwa: 12/07/2024