Nimepata khabari kwamba kuna mtu alitoa mawaidha juu ya mlima ambapo akaulizwa mtazamo wake juu ya makundi mbalimbali. Jawabu lake ilikuwa kwamba kuna makubaliano baina yao kwamba wamoja wasiwazungumze wengine. Hii ndio athari ya Hizbiyyah, utawala na tamaa za kidunia. Kwa ajili hiyo namnasihi kila mwanafunzi ajiepushe na vyama hivi na kuwatahadharisha waislamu kutokamana nao kwa kila hali na kila njia; kwa kuandika, kuzungumza, mihadhara, mahojiano na mijadala ya hadhara, ili jamii iwaone kuwa watu hawa hawashikamani na dini kama inavyopasa.

Mambo yanahusiana na tamaa za kidunia na maslahi. Sisi tunaweza kujinusuru kwa njia ya kwamba tunaweza kuwa au kufanya tutakavyo? Hapana. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

إِن يَنصُرْكُمُ اللَّـهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ ۖ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ

”Akikunusuruni Allaah, basi hakuna wa kukushindeni, na akikukosesheni nusura, basi nani atakunusuruni baada Yake? – na kwa Allaah pekee wanategemea waumini.”[1]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّـهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ

“Enyi mloamini! Mkisaidia kuinusuru dini ya Allaah, basi atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.”[2]

Hatuwezi kujisiaida wenyewe kwa njia ya kwamba tukawa, tukaficha baadhi ya elimu au tukanyamazia baadhi ya maudhui ili tusiwakimbize watu. Mola amemwambia Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ

”Ee Mtume! Fikisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako na usipofanya, basi utakuwa hukufikisha ujumbe Wake; na Allaah atakuhifadhi na watu. Hakika Allaah hawaongozi watu makafiri.”[3]

Sisi si wenye kufanya vurugu katika dini hii kwa njia ya kwamba tukachelewesha baadhi ya mambo na kuyanyamazia mengine. Pengine baadhi ya mambo yakawa ni shirki. Je, watatunyamazisha mpaka watakapopata utawala? Kisha nini wanachofanya wakati wanapopata utawala?

[1] 03:160

[2] 47:7

[3] 05:67

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 387-388
  • Imechapishwa: 19/06/2025