Hatutakiwi kuhisi upweke. Mara nyingi Ahl-us-Sunnah siku zote mna kila pahali wanakuwa wachache. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ

“Tendeni, enyi familia ya Daawuud, kwa shukurani!” Na ni wachache miongoni mwa waja Wangu wenye kushukuru.”[1]

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ

”Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza Njia ya Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa ila wenye kubuni uongo.”[2]

وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ

“Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi.”[3]

Wachache ndio ambao Allaah (Ta´ala) anawafanya imara. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakutoacha kuwepo kikundi katika Ummah wangu kuwa juu ya haki waziwazi. Hakitodhurika na wale wenye kuwakosesha nusura na wale wenye kwenda kinyume nao mpaka ifike amri ya Allaah ilihali wako katika hali hiyo.”[4]

Wengi ni wale wenye kushikamana na haki ijapo atakuwa ni mtu mmoja tu. Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) alibaki imara kipindi ambacho wengi walirudi nyuma. Baada ya Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) pia wanaobaki imara ni wachache. ´Aliy bin al-Husayn amesema:

“Nilimuuliza ´Abdullaah bin al-Mubaarak: “Mkusanyiko ni wepi?” Akajibu: “Ni Abu Bakr na ´Umar.” Kukasemwa: “Lakini wamefichikana.” Ndipo akasema: “Ni fulani na fulani na fulani na fulani.” Kukasemwa: “Lakini hao pia wamefichikana.” Ndipo ´Abdullaah bin al-Mubaarak akasema: “Abu Hamzah as-Sukkariy ndiye Mkusanyiko.”[5]

 Kwa hiyo muislamu hatakiwi kuhisi upweke muda wa kuwa ameshikamana na haki – hata kama atabaki mwenyewe:

إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِّلَّـهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ

”Hakika Ibraahiym alikuwa ni mfano mwema, mnyenyekevu kwa Allaah na mwenye kuelemea Tawhiyd na kujiengua na shirki; hakuwa miongoni mwa washirikina.”[6]

Unachotakiwa ni wewe kutosheka na Qur-aan na Sunnah. Wale wanaoenda kinyume navyo hawatokudhuru chochote muda wa kuwa umetosheka na Qur-aan an Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pepo imezungukwa na matatizo na Moto umezungukwa na matamanio.”[7]

Mapote haya yanawakusanya wafuasi wao kwa ajili ya maslahi. Wewe, ee Sunniy, uko pamoja na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Usiruhusu dhoruba hizi zikakushtua. Zitaondoka na kutabaki Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 34:13

[2] 06:116

[3] 12:103

[4] Muslim (1920).

[5] at-Tirmidhiy (2167).

[6] 16:120

[7] Muslim (2822).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 383-384
  • Imechapishwa: 19/06/2025