Swali: Kuhusiana na masomo, wanasema kuwa wanarejea kwa Shaykh [Muhammad] Naaswir[-ud-Diyn al-Albaaniy] inapokuja katika uanishaji wa Hadiyth…

al-Albaaniy: Allaah ni Mkubwa. Hili linanikumbushia Hizb-ut-Tahriyr wakati nilipojadiliana nao Dameski. Niliwaambia kuwa wanataka kusimamisha dola ya Kiislamu tangu Taqiyy-ud-Diyn an-Nabhaaniy alipounda hukumu kwenye kitabu “Nidhwaam-ul-Hukm” juu ya Hadiyth dhaifu na zisizokuwa na asli. Vipi mnataka kusimamisha dola wakati hamna hata katiba ya dola ilio wazi? Mnarejea kwangu ilihali mnanichukulia kama mpinzani? Vipi mnakubali maneno yangu juu ya kwamba Hadiyth ni Swahiyh au dhaifu?

Haya uliyosema sasa hivi yanathibitisha yale niliyosema karibuni; hawakusoma Qur-aan kwa mujibu wa Sunnah na hawakusoma Sunnah kutokana na mafundisho ya Hadiyth, istilahi ya Hadiyth na ukosoaji na kusifia. Kwa neno “fikra huru” wanachomaanisha ni kujitoa katika hukumu za Qur-aan na Sunnah Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (951)
  • Imechapishwa: 30/08/2020