Swali: Ni ipi hukumu ya kunyo ndevu na kuzipunguza? Je, kitendo cha Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ni hoja?
Jibu: Kunyoa ndevu ni haramu. Anyenyoa ndevu anazingatiwa kuwa ni mtenda dhambi nzito. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jitofautisheni na washirikina! Punguzeni masharubu na fugeni ndevu.”[1]
Ni dhambi pia kupunguza, kutegemea na kile kiasi ambacho mtu amepunguza. Ndevu zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zilikuwa zinafunika kifua chake. Muislamu anatakiwa kuziachia ndevu zake kama alivyotaka Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ndevu zinahesabiwa ni utukufu na uanaume. Aidha ndevu zinahesabiwa ni heshima kwa njia ya kwamba mtenda dhambi hathubutu kutenda dhambi mbele ya mwanaume mwenye ndevu.
Kitendo cha Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) sio hoja. Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ
“Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu na wala msifuate badala Yake wasaidizi wengine. Ni machache mnayoyakumbuka!”[2]
[1] al-Bukhaariy, Muslim, Abu ´Awaanah na al-Bayhaqiy kupitia kwa Naafiy´.
[2] 7:3
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 317
- Imechapishwa: 21/05/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket