Swali: Watu wengi wanapofanya maasi na wakasimamishiwa adhabu wakaingia gerezani, husema: “Hii ni mipango na makadirio ya Allaah na wanamshukuru Allaah kuwa amewakadiria hivi.” Je, hilo likoje?
Jibu: Ndiyo, hilo limeandikwa na Allaah. Lakini pamoja na hayo ni lazima atubie. Ni mipango na makadirio, lakini anawajibika kutubia. Amshukuru Allaah kwa yale aliyokadiria, kwa kuwa amepewa adhabu yake, kusimamishiwa adhabu ya kidini na kwa kusubiri juu ya yale aliyoyakadiria Allaah na aridhike na mipango ya Allaah. Lakini pamoja na hayo ni lazima aharakishe kutubia, kujuta, kuacha dhambi hiyo na kuazimia kutorudia tena. Makadirio ya Allaah hayapaswi kumfanya aendelee kung’ang’ania maasi au kurudia dhambi. Badala yake makadirio yanapaswa kumfariji nafsi yake, kumfanya amshukuru Allaah kwa aliyoyakadiria, kwa kuwa amepewa adhabu na ametubia kwa Allaah na amerudi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Wala asifanye makadirio kuwa ni hoja ya kuhalalisha maasi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3432/وجوب-الايمان-بالقدر-للمذنب-مع-التوبة
- Imechapishwa: 22/08/2026
Swali: Watu wengi wanapofanya maasi na wakasimamishiwa adhabu wakaingia gerezani, husema: “Hii ni mipango na makadirio ya Allaah na wanamshukuru Allaah kuwa amewakadiria hivi.” Je, hilo likoje?
Jibu: Ndiyo, hilo limeandikwa na Allaah. Lakini pamoja na hayo ni lazima atubie. Ni mipango na makadirio, lakini anawajibika kutubia. Amshukuru Allaah kwa yale aliyokadiria, kwa kuwa amepewa adhabu yake, kusimamishiwa adhabu ya kidini na kwa kusubiri juu ya yale aliyoyakadiria Allaah na aridhike na mipango ya Allaah. Lakini pamoja na hayo ni lazima aharakishe kutubia, kujuta, kuacha dhambi hiyo na kuazimia kutorudia tena. Makadirio ya Allaah hayapaswi kumfanya aendelee kung’ang’ania maasi au kurudia dhambi. Badala yake makadirio yanapaswa kumfariji nafsi yake, kumfanya amshukuru Allaah kwa aliyoyakadiria, kwa kuwa amepewa adhabu na ametubia kwa Allaah na amerudi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Wala asifanye makadirio kuwa ni hoja ya kuhalalisha maasi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3432/وجوب-الايمان-بالقدر-للمذنب-مع-التوبة
Imechapishwa: 22/08/2026
https://firqatunnajia.com/nasibisha-janga-lililokufika-na-makadirio-ya-allaah-pamoja-na-kutubia/