Swali: Nimeomba kazi katika hospitali kama mtafsiri na katika hospitali hii kama zilivyo hospitali nyingine kuna kuchanganyika kati ya wanaume na wanawake. Swali langu ni kwa sababu ya kazi yangu ninalazimika kuchanganyika na wanawake wagonjwa na wafanyakazi. Ni yepi maoni yenu kuhusu jambo hili? Nifahamisheni – Allaah awalipe kheri – hali ya kuwa nina uhitaji mkubwa wa kazi hii?
Jibu: Ikiwa kazi yako inakufanya uchanganyike na wanawake, basi jiepushe na jihadhari usije ukapata madhara amapo shaytwaan akakupata kupitia wao. Kwa hiyo jihadhari. Ama ikiwa kazi yako iko mbali nao, kwa maana wewe ni mtafsiri tu kwa yale yanayoletwa kwako na kufikishwa kwako katika ofisi yako, unatafsiri na kuwapa, basi hakuna ubaya. Lakini ikiwa utachanganyika na wanawake, wagonjwa na wasiokuwa wagonjwa, huenda hilo likakusababishia matatizo mengi na khatari nyingi. Wanawake hao wanaweza kuwa karibu uchi na wengi wao hawajali kujisitiri na Hijaab au wote, basi uko katika khatari. Kwa hivyo jihadhari na jiepushe na riziki iko kwa Allaah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3414/حكم-العمل-في-اماكن-الاختلاط
- Imechapishwa: 21/08/2026
Swali: Nimeomba kazi katika hospitali kama mtafsiri na katika hospitali hii kama zilivyo hospitali nyingine kuna kuchanganyika kati ya wanaume na wanawake. Swali langu ni kwa sababu ya kazi yangu ninalazimika kuchanganyika na wanawake wagonjwa na wafanyakazi. Ni yepi maoni yenu kuhusu jambo hili? Nifahamisheni – Allaah awalipe kheri – hali ya kuwa nina uhitaji mkubwa wa kazi hii?
Jibu: Ikiwa kazi yako inakufanya uchanganyike na wanawake, basi jiepushe na jihadhari usije ukapata madhara amapo shaytwaan akakupata kupitia wao. Kwa hiyo jihadhari. Ama ikiwa kazi yako iko mbali nao, kwa maana wewe ni mtafsiri tu kwa yale yanayoletwa kwako na kufikishwa kwako katika ofisi yako, unatafsiri na kuwapa, basi hakuna ubaya. Lakini ikiwa utachanganyika na wanawake, wagonjwa na wasiokuwa wagonjwa, huenda hilo likakusababishia matatizo mengi na khatari nyingi. Wanawake hao wanaweza kuwa karibu uchi na wengi wao hawajali kujisitiri na Hijaab au wote, basi uko katika khatari. Kwa hivyo jihadhari na jiepushe na riziki iko kwa Allaah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3414/حكم-العمل-في-اماكن-الاختلاط
Imechapishwa: 21/08/2026
https://firqatunnajia.com/nifanye-nini-ikiwa-kazi-pekee-niliyopata-ni-ya-kuchanganyikana-na-wanawake/