Inafaa kwa muislamu kushirikiana na kafiri katika mambo biashara?

Swali: Je, inajuzu kwa muislamu kushirikiana na kafiri katika miradi ya biashara au makandarasi?

Jibu: Inajuzu ikiwa haitahusisha uovu wala shari, kuhalalisha kilichoharamishwa, kumfanya kuwa rafiki wa karibu au kumpa utii na mapenzi ya ndani. Hata hivyo kuacha kushirikiana naye ni salama zaidi. Kwa msemo mwingine muislamu kushirikiana na waislamu wenzake na kuchagua mshirika muislamu ni bora na ni tahadhari zaidi. Kwa sababu hiyo baadhi ya wanazuoni wameona ni machukizo ya kushirikiana na kafiri. Lakini ikiwa atafanya ushirika huo, basi ni sahihi mradi asifanye mambo yaliyoharamishwa kama kumpenda kwa mapenzi ya kidini na kumpa utii na urafiki wa karibu unaopingana na misingi ya dini. Hivyo ikiwa ni ushirika wa mali tu kwa lengo la kupata faida, bila kuwepo urafiki wa karibu, mapenzi ya kidini au utii usiofaa, basi hakuna ubaya. Lakini wajibu unabaki kuwa ni kumchukia kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3420/حكم-مشاركة-المسلم-للكافر-في-المشاريع-التجارية
  • Imechapishwa: 22/08/2026