Mama amemuua mtoto kwa kuweka dawa mahali pasipotakiwa

Swali: Nina dada yangu aliyekwenda hospitali na aliporudi alikuwa na haraka, akaweka dawa mahali pasipo salama. Alikuwa na mtoto mdogo ambaye akala hiyo dawa hadi akafa. Tunaomba mumkinaishe ili aridhike nafsi yake, kwani anasema kuwa amefanya dhambi. Je, anaadhibiwa kwa adhabu yoyote au kuna kafara juu yake ilihali hakukusudia?

Jibu: Tunatarajia asiwe na dhambi, kwa sababu hakukusudia kumuua wala hakukusudia kusababisha hilo. Bali alighafilika au alisahau khatari ambapo akaweka dawa mahali pasipofaa ambapo watoto wanaweza kufikia.

Lakini kinachoonekana ni kwamba juu yake kuna fidia ya damu na kafara, kwa sababu alifanya uzembe kwa kuiweka mahali karibu na watoto wadogo wasio na ufahamu. Ilimpasa aiweke mahali pa juu au mbali na watoto.

Ama kuhusu dhambi, tunatarajia hana dhambi kwa kuwa hakukusudia ubaya. Bali ni kughafilika au kusahau kulikosababisha kuweka dawa mahali pasipofaa. Hata hivyo juu yake kuna fidia ya damu na kafara, isipokuwa kama warithi watamsamehe kuhusu diyah, basi hakuna tatizo. Ama kafara ni kuacha huru mtumwa muumini. Ikiwa hatapata, basi afunge miezi miwili mfululizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3426/حكم-الام-اذا-كانت-سببا-في-قتل-طفلها-دون-قصد
  • Imechapishwa: 22/08/2026