Nasaha kwa wanafunzi wanaowadhania vibaya wanafunzi wenzao

Swali: Baadhi ya wanafunzi wanaohudhuria darsa hizi hawatoi salamu, bali hata hawajibu salamu za wanafunzi wengine wanaohudhuria mara kwa mara, ingawa hatukuona kutoka kwao isipokuwa kheri na hakuna shari iliyoonekana kwao. Ikiwa hawa wamejenga kitendo chao juu ya yakini na uthibitisho, basi watubainishie ili tufikie lengo la nasaha, ukumbusho na kukataza maovu. Ikiwa wametegemea dhana, mawazo na tuhuma, basi tunatarajia uwape?

Jibu: Ni wajibu kwa muumini kuwa na dhana njema kwa ndugu yake, kushirikiana naye katika wema na uchaji na kuusiana juu ya haki na kusubiri juu yake. Huu ndio wajibu wa wote, kama Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ

“Hakika si vyenginevyo waumini ni ndugu.”[1]

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao; wanaamrisha mema na wanakataza maovu.”[2]

وَالْعَصْرِ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ

”Naapa kwa al-‘Aswr. Hakika ya mwanaadamu bila ya shaka yumo katika khasara. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana kwa kufuata ya haki na wakausiana kuwa na subira.”[3]

وَالْعَصْرِ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ

”Naapa kwa al-‘Aswr. Hakika ya mwanaadamu bila ya shaka yumo katika khasara. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana kwa kufuata ya haki na wakausiana kuwa na subira.”[4]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema alipoulizwa:

”Ni Uislamu upi bora?” Akasema: ”Ni kulisha chakula na kusoma salamu kwa yule umjuaye na usiyemjua.”

Kwa hiyo ni wajibu kupendana kwa ajili ya Allaah, kushirikiana katika kheri, kushirikiana katika haki na subira juu yake, na kuchukua tahadhari na mambo yanayosababisha ghadhabu ya Allaah.

[1] 49:10

[2] 09:71

[3] 103:1-3

[4] 103:1-3

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31016/ما-النصيحة-لمن-لا-يحسنون-الظن-بالناس
  • Imechapishwa: 28/09/2025