Swali: Mke wangu anaswali Nawaafil nyingi za swawm, swalah na kusoma Qur-aan. Lakini hata hivyo hajihimizi kumtii mume wake na khaswa upande wa kitandani. Naomba umnasihi.
Jibu: Ninamnasihi mke wake kumtii mume wake kwa kuwa ni katika kumtii Allaah. Atekeleze haki zake na asimuasi katika wema. Atekeleze maombi yake kwa kuwa hili ni katika kumtii Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema katika Hadiyth Swahiyh:
“Mwanamke akiswali vitano vyake, akafunga mwezi wake, akamtii mume wake na akahifadhi tupu yake, basi ataambiwa [siku ya Qiyaamah]: “Ingia Peponi kwa mlango wowote unaoutaka.””
Mwanamke huyu amefanya mapungufu katika haki za mume wake. Hivyo kunakhofiwa juu yake asipate hili. Ninamnasihi mwanamke huyu atubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na atekeleze haki za mume wake na asichelewe kumtekelezea maombi yake. Amtii katika mema.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://shrajhi.com//Live/ArID/339
- Imechapishwa: 19/09/2020
Swali: Mke wangu anaswali Nawaafil nyingi za swawm, swalah na kusoma Qur-aan. Lakini hata hivyo hajihimizi kumtii mume wake na khaswa upande wa kitandani. Naomba umnasihi.
Jibu: Ninamnasihi mke wake kumtii mume wake kwa kuwa ni katika kumtii Allaah. Atekeleze haki zake na asimuasi katika wema. Atekeleze maombi yake kwa kuwa hili ni katika kumtii Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema katika Hadiyth Swahiyh:
“Mwanamke akiswali vitano vyake, akafunga mwezi wake, akamtii mume wake na akahifadhi tupu yake, basi ataambiwa [siku ya Qiyaamah]: “Ingia Peponi kwa mlango wowote unaoutaka.””
Mwanamke huyu amefanya mapungufu katika haki za mume wake. Hivyo kunakhofiwa juu yake asipate hili. Ninamnasihi mwanamke huyu atubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na atekeleze haki za mume wake na asichelewe kumtekelezea maombi yake. Amtii katika mema.
Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://shrajhi.com//Live/ArID/339
Imechapishwa: 19/09/2020
https://firqatunnajia.com/nasaha-kwa-mwanamke-mchaji-asiyemtii-mume-wake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)