Nasaha kwa mwanafunzi anayetaka kuoa na hana uwezo

Swali: Ni ipi nasaha yako kwa mwanafunzi anayesoma katika chuo kikuu na hana cha kumtosheleza ili aweze kuoa, lakini wakati huohuo ana khofu juu ya nafsi yake?

Jibu:

وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ

”Na watafute sitara [ya kujizuia na machafu] wale ambao hawapati ndoa mpaka Allaah awatajirishe katika fadhilah Zake.” (24:33)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Enyi kongamano la vijana! Yule mwenye uwezo wa kuoa na afanye hivyo, kwani hilo linamfanya ainamishe macho yake na inahifadhi utupu wake. Ama kwa yule asiyeweza basi afunge, kwani kufanya hivyo ni kinga kwake.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14301
  • Imechapishwa: 17/11/2014