Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

07- Abu Ruqayyah Tamiym bin Aws ad-Daariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dini ni nasaha.” Tukauliza: “Kwa nani?” Akasema kwa Allaah, Kitabu Chake, Mtume Wake, kwa Viongozi wa Waislamu na watu wa kawaida.”

Kumnasihi mtawala inatakiwa iwe kwa siri na isiwe hadharani. Kwa sababu asli ya nasaha kwa dhati yake, sawa ikiwa ni kwa mtawala au kwa mwengine, inatakiwa iwe kwa siri. Hili ni tofauti na kukataza, kama itakavokuja huko mbele wakati wa kufafanua Hadiyth ya Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh):

“Mwenye kuona maovu katika nyinyi basi ayazuie kwa mkono wake…”

Asli katika kukataza inakuwa hadharani. Ama kuhusu nasaha inakuwa kwa siri.

Nasaha kwa mtawala ni wajibu na imeshurutishwa iwe kwa siri, bi maana asiwepo mwingine atakayejua hilo isipokuwa yeye mwenyewe na asielezee juu ya hilo ya kwamba amemnasihi na kadhalika. Kwa sababu huenda akaharibu malengo na hivyo ikawa ni vigumu kukubali nasaha hiyo baada ya kusema hadharani ya kwamba amemnasihi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 165
  • Imechapishwa: 17/05/2020