Swali: Tulimtuhumu ndugu yetu katika dini kwa baadhi ya mambo yaliyoharamishwa na ili tujihakikishie tukakutana mara moja nyumbani pamoja na baadhi ya ndugu zetu katika dini, na ikatokea akaja huyo mtu ambaye tulikuwa tunamhesabu kuwa ni mwenye msimamo, lakini tulisikia kutoka kwa baadhi ya watu wakimtuhumu kwa baadhi ya mambo yaliyoharamishwa. Alipokuja kwetu tukaanza kuzungumza kuhusu baadhi ya mambo hayo yaliyoharamishwa, kisha tukazungumza naye ili tumjaribu kama ameathirika na maneno hayo au hapana? Tukatumia baadhi ya mifano na mafumbo na tukaona uso wake umebadilika kidogo, kisha baada ya hapo hakurudi kwetu. Tulikusudia kwa hilo kujihakikishia uhusiano wa mambo hayo kwake na wakati huohuo kumpa nasaha, lakini inaonekana hakukubali maneno yetu; kwa sababu tulikuwa tunatumia mifano, mafumbo na nasaha mbele ya kikao kilichotujumuisha. Je, sisi tumekosea au tumepatia katika njia yetu hii ya kuamrisha mema na kukataza maovu?
Jibu: Kwa vyovyote vile wajibu juu ya wanazuoni na juu ya ndugu wao baina yao ni kushauriana na kusaidiana juu ya wema na kumcha Allaah. Ikiwa inawezekana mtu kumnasihi kwa faragha akiwa peke yake, muda wa kuwa hajatangaza, basi inafaa kumnasihi peke yake na kuwasiliana naye kutoka kwa baadhi ya ndugu zake peke yake bila kueneza kati ya watu. Kwa sababu aliposikia maneno alidhani kuwa analengwa, ndio maana akabadilika.
Ninachotaka kusema ni kwamba mfano wa hili muda wa kuwa mtu hajaanika maasi na hayajaonekana kutoka kwake, basi inafaa nasaha yake iwe siri kati yako na yeye ili asidhani kuwa anatuhumiwa mbele ya watu na kwamba anajulikana kwa maovu mbele ya watu, hali yeye hakufanya hayo, wala hakuyatangaza wala hakuyadhihirisha. Bali ni tuhuma na dhana. Huenda ikawa ni dhana mbaya. Kwa hiyo inafaa kwa muumini katika mambo kama haya nasaha yake iwe ya siri kati yake na ndugu yake. Huenda Allaah akamnufaisha kwa hilo, kwani nasaha ya siri ina athari kubwa.
Ama ikiwa ameonyesha uovu, basi akemewe waziwazi hakuna ubaya. Ikiwa anajulikana kwa uovu huo, kama kuchelewa swalah, kutumia vilevi waziwazi, kunyoa ndevu – kunyoa ndevu ni jambo lililo wazi – na mfano wa hayo, jambo lililo wazi hukemewa waziwazi. Ama yale yanayodhaniwa kwa dhana tu, basi inafaa yawe kati yako na yeye na utumie maneno mazuri: mimi ninaogopa hili na imenifikia kwamba. Unamwambia maneno yanayofaa. Inafaa kwako ikiwa unafanya jambo hili uache, ujihadhari nalo, ee ndugu yangu, umche Allaah na ujue kuwa anakuchunga na mfano wa maneno ambayo yanakuwa ya kuzingatiwa. Huenda yakamwathiri athari kubwa, kwa sababu umemnasihi kwa siri na umekaa naye peke yake na umemtembelea mahali pake au mahali maalum. Nataraji Allaah atanufaisha kwa hilo. Ama kutangaza bila kuonekana maasi na bila kuonekana Bid´ah, basi hili linaogopwa kuwa na majibu yasiyofaa, kwa maana kunakhofiwa kuwa kinyume chake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3362/كيفية-نصيحة-من-ظن-به-السوء
- Imechapishwa: 20/09/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3362/كيفية-نصيحة-من-ظن-به-السوء
Imechapishwa: 20/09/2026
https://firqatunnajia.com/nasaha-kwa-anayedhaniwa-kufanya-maovu/