182 – Ibraahiym bin Ya´quub ametuhadithia: Ishaaq bin Ya´quub bin Ishaaq ametukhabarisha: ´Affaan ametukhabarisha: Hammaad bin Salamah ametukhabarisha: Thaabit ametukhabarisha, kutok akwa Mu´aawiyah bin Qurrah, kutoka kwa ´Aa-idh bin ´Amr, amabye ameeleza:
“Abu Sufyaan akapita karibu na Salmaan, Swuhayb na Bilaal waliokuwa wameketi chini na kusema: “Upanga wa Allaah bado haujafanya kazi yake kwa maadui wa Allaah.” Abu Bakr akasema: “Je, unasema hivyo kuhusu mkuu na kiongozi wa Quraysh?” Akamwendea Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kumjulisha. Akasema: “Ee Abu Bakr, labda umewakasirisha? Ikiwa umewakasirisha, basi umemkasirisha Mola wako.” Akarejea na kusema: “Enyi ndugu zangu! Labda nimekukasirisheni?” Wakasema: “Hapana, Abu Bakr. Allaah akusamehe.”[1]
Tamko ni la Ibraahiym.
183 – Qutaybah bin Sa´iyd ametukhabarisha: ´Abdul-´Aziyz ametuhadithia, kutoka kwa Thawr, kutoka kwa Abul-Ghayth, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye ameeleza:
“Tulipokuwa tumekaa kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wakati ilipoteremshwa kwake Suurah “al-Jumu’ah.” Wakati aliposoma:
وَآخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا بِهِمْ
“Wengineo ambao bado hawajakutana nao.”[2]
akasema mtu mmoja: “Ni kina nani hao, ee Mtume wa Allaah?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) hakumjibu mpaka alipomuuliza mara mbili au mara tatu. Salmaan alikuwa kati yetu. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akauweka mkono wake juu ya Salmaan na akasema: “Lau kuwa imani ingekuwa katika Kilimia, basi angeliipata mtu kutoka katika watu hawa.”[3]
[1] Muslim (2504).
[2] 62:3
[3] al-Bukhaariy (4897) na Muslim (2546).
- Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 115-116
- Imechapishwa: 20/09/2026

Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 115-116
Imechapishwa: 20/09/2026
https://firqatunnajia.com/fadhilah-za-swuhayb-bin-sinaan/