Nani bora kumpa zakaah katika hawa watatu?

Swali: Bora kuwapa zakaah mafukara, wenye deni au wanaopigana jihaad katika njia ya Allaah?

Jibu: Wote ni watu wanastahiki kupewa zakaah. Akiwapa mafukara wanastahiki. Akiwapa wenye deni wasiokuwa na uwezo wanastahiki. Akiwapa wanaopigana jihaad katika njia ya Allaah wanastahiki. Wote wanapewa kutegemea na haja. Bora kuwapa wanaopambana jihaad ikiwa ni wahitaji. Ikiwa mafukara wana haja kubwa wataokolewa kwa zakaah wasife. Hali inatofautiana. Ajitahidi.

Swali: Vipi akiigawanya kati yao?

Jibu: Yote yanafaa. Amepewa khiyari; akitaka atawapa hawa au hawa. Upande wowote katika hawa wanaofuata atawapa basi imesihi; mafukara, katika njia ya Allaah, wenye deni, kuacha mtumwa huru au wale zinaolainishwa nyoyo zao [katika Uislamu], kama alivobainisha Allaah (Subhaanah). Jambo ni lenye wasaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22769/ما-الافضل-في-الزكاة-للفقير-والمدين-والجهاد
  • Imechapishwa: 19/08/2023