Swali: Nina binamu ambaye ameshazaa watoto saba na hali yake ya kifedha ni dhaifu. Nami nina uwezo wa kumsaidia. Nina mke ambaye kila anapojua kwamba nimemtumia pesa, hunikasirikia kwa hasira kali na huacha kula na swalah kwa muda wa miaka mitano katika hali hii. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Huyu ni mke mwenye kufanya dhuluma – tunamuomba Allaah atupe usalama. Hapaswi kumtii katika jambo hili. Anatakiwa kutoa swadaqah kwa binamu yake na kumfanyia wema. Huenda ana wasichana na yeye anaogopa kwamba huenda akaoa miongoni mwao; pengine ana msichana na anaogopa jambo hilo. Mwanamke huyu ni mwenye dhana mbaya.

Tunachokusudia ni kwamba atunze jambo hili na amsaidie na amfanyie wema bila yeye kujua. Asimweleze. Afanye kwa njia nyingine ili kukusanya maslahi mawili. Anaweza kutoa swadaqah kwa njia nyingine, kwa njia ya siri, bila kumjulisha chochote. Pia amnasihi kwa ajili ya Allaah na amukhofishe Allaah. Ikiwa haswali, inamlazimu kuachana naye. Hana kheri. Pamoja na hayo, anamsaidia katika kukata undugu wa jamaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1960/نصيحة-لزوجة-لا-تعين-زوجها-على-بر-اقاربه
  • Imechapishwa: 25/07/2026