Ameweka nadhiri ya kufunga miaka miwili iwapo atafanya punyeto

Swali: Niliweka nadhiri kwamba nikijitoa manii kwa mkono nitafunga miaka miwili mfululizo kwa lengo la kujizuia na tabia hii. Lakini nimeifanya na siwezi kufunga. Nifanye nini?

Jibu: Nadhiri hii imechukizwa na haifai. Kwa sababu ni nadhiri ambayo si ya kujikurubisha kwa Allaah, bali ni ya kujizuia na tabia hii. Ni kama mtu anayesema ”Nikizungumza na fulani nitafunga miaka” au ”Nikimtembelea nitafunga miaka miwili”. Maana yake ni kujihimiza kuacha au kujizuia na jambo fulani. Hukumu yake ni kama hukumu ya kiapo. Hapana juu yake kufunga. Anatakiwa kulisha chakula masikini kumi au kuwavisha nguo na hilo linatosha. Wala si juu yake kufunga miaka hiyo miwili, kwa sababu lengo lake halikuwa kujikurubisha. Bali lilikuwa kujizuia na jambo hilo.

Ni lazima ajihadhari na tabia ya kujitoa manii nayo kabisa, hata kama hakuweka nadhiri. Ni wajibu ajiepushe nayo. Aidha ni wajibu asilenge macho yake kwa wanawake, ateremsha chini macho yake kutokana na wanawake na kwa wavulana na pia awe na tahadhari, amuogope Allaah, Allaah anamchunga. Aidha afunge kwa wingi, ajikaribishe na mke wake ikiwa ana mke au aoe. Kwa kuyafanya haya itaondoka shari pamoja na tiba. Kila maradhi yana dawa:

”Allaah hakuteremsha maradhi yoyote isipokuwa ameteremsha pia dawa yake.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1948/كفارة-النذر-المكروه
  • Imechapishwa: 25/07/2026