Swali: Kuna mgonjwa wa kupooza ambaye hawezi kutembea bila kifaa cha kitabibu. Kifaa hicho kina mikanda ya ngozi yenye kushonwa kwa nyuzi na pia kuna viatu. Je, ni ipi hukumu ya kuingia katika Ihraam ya Hajj huku akiwa na haja ya kuvaa kifaa hicho katika kipindi chote cha Ihraam?
Jibu: Hilo halina madhara. Nyuzi zilizoshonwa na mkanda kwa mwenye kuhiji havidhuru. Hakuna kosa juu yake kwa sababu ya hali ya dharurah.
Vivyo hivyo viatu, kwani mwenye kuingia katika Ihraam anaruhusiwa kuvaa viatu. Hata asiwe mgonjwa, kuvaa viatu viwili kunaruhusiwa kwa aliye katika Ihraam na hivyo hakuna tatizo katika hilo.
Kilichokatazwa ni mavazi ya kawaida yaliyoshonwa yanayovaliwa kama nguo za kila siku, kama vile suruwali ya kawaida, shati au kufunika kichwa. Haya ndiyo yaliyokatazwa kwa aliye katika Ihraam.
Ama kufunga mkanda au kifaa kwenye mkono au miguuni kwa sababu ya maradhi yake au kuvaa viatu miguuni, basi hayo hayana madhara kwa aliye katika Ihraam. Hayamdhuru mwenye Ihraam hata kama angekuwa si mgonjwa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1951/حكم-لبس-المحرم-المخيط-للحاجة
- Imechapishwa: 25/07/2026
Swali: Kuna mgonjwa wa kupooza ambaye hawezi kutembea bila kifaa cha kitabibu. Kifaa hicho kina mikanda ya ngozi yenye kushonwa kwa nyuzi na pia kuna viatu. Je, ni ipi hukumu ya kuingia katika Ihraam ya Hajj huku akiwa na haja ya kuvaa kifaa hicho katika kipindi chote cha Ihraam?
Jibu: Hilo halina madhara. Nyuzi zilizoshonwa na mkanda kwa mwenye kuhiji havidhuru. Hakuna kosa juu yake kwa sababu ya hali ya dharurah.
Vivyo hivyo viatu, kwani mwenye kuingia katika Ihraam anaruhusiwa kuvaa viatu. Hata asiwe mgonjwa, kuvaa viatu viwili kunaruhusiwa kwa aliye katika Ihraam na hivyo hakuna tatizo katika hilo.
Kilichokatazwa ni mavazi ya kawaida yaliyoshonwa yanayovaliwa kama nguo za kila siku, kama vile suruwali ya kawaida, shati au kufunika kichwa. Haya ndiyo yaliyokatazwa kwa aliye katika Ihraam.
Ama kufunga mkanda au kifaa kwenye mkono au miguuni kwa sababu ya maradhi yake au kuvaa viatu miguuni, basi hayo hayana madhara kwa aliye katika Ihraam. Hayamdhuru mwenye Ihraam hata kama angekuwa si mgonjwa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1951/حكم-لبس-المحرم-المخيط-للحاجة
Imechapishwa: 25/07/2026
https://firqatunnajia.com/muhrim-kuvaa-mavazi-yaliyoshonwa-kwa-sababu-ya-haja/