Swali: Mimi nimenunua magari kumi kutoka kwenye maonyesho ya magari, nikayaacha pale pale kwenye maonyesho na sikutoa gari hata moja. Nikatoa pesa zake zote na wala sikuyahamishia kwa jina langu kabisa. Kila nilipopata mteja nilimuuzia gari lilelile, nalo likiwa bado mahali pake. Kwa maana nyingine sikuhamisha gari hata moja wala sikuliondoa, nililipa pesa tu. Biashara na ununuzi huu ukoje?
Jibu: Inapaswa uyahamisha kutoka mahali pa kuuza kwenda mahali pengine, kwenda kwenye maonyesho mengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuuzwa bidhaa mahali iliponunuliwa mpaka wafanyabiashara waihamishe kwenda kwenye maeneo yao. Kwa hiyo haifai uyauze yakiwa bado kwenye maonyesho uliyoyanunulia. Bali uyahamishie kwenye maonyesho mengine, nyumbani kwako au kwenye soko jingine miongoni mwa masoko ya waislamu. Wala usiyauze yakiwa bado mahali pake, kwa kutekeleza maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa kufuata mwongozo wake katika kutokuuza bidhaa mahali ziliponunuliwa.
Swali: Lakini nilikubaliana naye kwamba yabaki pale mpaka tutakapomaliza mambo ya mahali hapo?
Jibu: Yabaki pale mpaka uyahamishie kwenye maonyesho mengine.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1954/بيع-ما-تم-شراوه-دون-نقله-من-مكان-الشراء
- Imechapishwa: 25/07/2026
Swali: Mimi nimenunua magari kumi kutoka kwenye maonyesho ya magari, nikayaacha pale pale kwenye maonyesho na sikutoa gari hata moja. Nikatoa pesa zake zote na wala sikuyahamishia kwa jina langu kabisa. Kila nilipopata mteja nilimuuzia gari lilelile, nalo likiwa bado mahali pake. Kwa maana nyingine sikuhamisha gari hata moja wala sikuliondoa, nililipa pesa tu. Biashara na ununuzi huu ukoje?
Jibu: Inapaswa uyahamisha kutoka mahali pa kuuza kwenda mahali pengine, kwenda kwenye maonyesho mengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuuzwa bidhaa mahali iliponunuliwa mpaka wafanyabiashara waihamishe kwenda kwenye maeneo yao. Kwa hiyo haifai uyauze yakiwa bado kwenye maonyesho uliyoyanunulia. Bali uyahamishie kwenye maonyesho mengine, nyumbani kwako au kwenye soko jingine miongoni mwa masoko ya waislamu. Wala usiyauze yakiwa bado mahali pake, kwa kutekeleza maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa kufuata mwongozo wake katika kutokuuza bidhaa mahali ziliponunuliwa.
Swali: Lakini nilikubaliana naye kwamba yabaki pale mpaka tutakapomaliza mambo ya mahali hapo?
Jibu: Yabaki pale mpaka uyahamishie kwenye maonyesho mengine.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1954/بيع-ما-تم-شراوه-دون-نقله-من-مكان-الشراء
Imechapishwa: 25/07/2026
https://firqatunnajia.com/kuuza-bidhaa-na-kuiuza-mahali-hapohapo-ulipoinunua/