Swali: Baadhi ya watenda maasi wanaposhauriwa wanamwambia mshauriji kwamba akafundishe msikitini.
Jibu: Hili ni miongoni mwa aina ya matendo ya wanafiki. Akemewe na afunzwe ya kwamba haijuzu kwake kusema hivo. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَإِذَا قِيلَ لَهُ اتَّقِ اللَّـهَ أَخَذَتْهُ الْعِزَّةُ بِالْإِثْمِ ۚ فَحَسْبُهُ جَهَنَّمُ ۚ وَلَبِئْسَ الْمِهَادُ
”Anapoambiwa: ”Mche Allaah”, basi hupandwa na kiburi kinachomfanya kutenda madhambi. Basi Jahannam inamtosheleza na mahali pabaya palioje pa kupumzikia!”[1]
Kilicho cha wajibu ni yeye kukubali haki na amwombe Allaah amzidishie kheri, amwombe Allaah amsaidie, amsamehe au amwongoze. Hivi ndivo anavyotakiwa kufanya mwenye kupewa mawaidha, sio kurudisha maneno mabaya kama kusema kwamba eti waachwe na dini yao au kwamba akafundishe msikitini. Yote haya ni kufanya kiburi na kupingana na haki.
[1] 02:206
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24237/حكم-من-لم-يقبل-النصيحة-وكيف-يعامل
- Imechapishwa: 16/09/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)