Swali: Kuhusu wasiwasi wa shaytwaan ndani ya swalah, je, mtu ageuze kichwa chake upande wa kushoto au akiinamishe kidogo ili apulize upande wa kushoto dhidi ya shaytwaan?
Jibu: Ageuze kidogo upande wa kushoto. Hivi ndivyo Sunnah ilivyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pale ´Uthman bin Abiy al-Aasw ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) alipomlalamikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Ee Mtume wa Allaah! Hakika shaytwaan ananichanganya katika swalah yangu.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Huyo ni shaytwaan anayeitwa ”Khinzab”. Ukihisi jambo hilo, basi puliza upande wako wa kushoto mara tatu na ujilinde kwa Allaah dhidi ya shaytwaan mara tatu.” ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) akasema: ”Nilifanya hivyo na Allaah akaondoa niliyokuwa nikihisi.”
Ameipokea Ahmad bin Hanbal pamoja na baadhi ya wanazuoni wa Sunan kwa cheni ya wapokezi Swahiyh[1].
[1] Ahmad (17440).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/340)
- Imechapishwa: 13/03/2026
Swali: Kuhusu wasiwasi wa shaytwaan ndani ya swalah, je, mtu ageuze kichwa chake upande wa kushoto au akiinamishe kidogo ili apulize upande wa kushoto dhidi ya shaytwaan?
Jibu: Ageuze kidogo upande wa kushoto. Hivi ndivyo Sunnah ilivyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pale ´Uthman bin Abiy al-Aasw ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) alipomlalamikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Ee Mtume wa Allaah! Hakika shaytwaan ananichanganya katika swalah yangu.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Huyo ni shaytwaan anayeitwa ”Khinzab”. Ukihisi jambo hilo, basi puliza upande wako wa kushoto mara tatu na ujilinde kwa Allaah dhidi ya shaytwaan mara tatu.” ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) akasema: ”Nilifanya hivyo na Allaah akaondoa niliyokuwa nikihisi.”
Ameipokea Ahmad bin Hanbal pamoja na baadhi ya wanazuoni wa Sunan kwa cheni ya wapokezi Swahiyh[1].
[1] Ahmad (17440).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/340)
Imechapishwa: 13/03/2026
https://firqatunnajia.com/namna-ya-kupuliza-ndani-ya-swalah-wakati-wa-kuhisi-wasiwasi/