Namna ya kuosha kapeti ya msikiti

Swali: Inatosheleza kunyunyizia maji kwenye kapeti ya msikiti ikipata mkojo, kwa kuzingatia ya kwamba kuna ugumu katika kuiosha?

Jibu: Vitu vyenye kuweza kutolewa sehemu na kupelekwa sehemu nyingine kama kapeti vinatakiwa kupelekwa sehemu na kuoshwa ili viwe visafi. Ama vitu vilivyo imara vilivyoambatana na ardhi vina hukumu moja kama ardhi. Katika hali hii vinatakiwa kunyunyiziwa maji na inatosheleza kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340204.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020