Namna ya kuoanisha Hadiyth mbili kuhusu du´aa

Swali: Kumepokelewa makatazo katika Sunnah juu ya kufungamanisha du´aa na matashi. Mtu asemeje kuhusu maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia mgonjwa:

لا بأس .. طهور إن شاء الله

“Hakuna neno [ugonjwa] ni kusafishwa na [madhambi] – Allaah akitaka.”

Jibu: Makatazo ya kufungamanisha du´aa na matashi ni mtu kusema:

“Ee Allaah! Nisamehe ukitaka.”

Kusema hivi ni kubaya zaidi kuliko kusema:

“Ee Allaah! Nisamehe – Allaah akitaka.” Hili ni mosi.

Pili: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لا بأس .. طهور إن شاء الله

“Hakuna neno [ugonjwa] ni kusafishwa na [madhambi] – Allaah akitaka.”

Haya ni maelezo. Ni kusafishwa kwa upande wa mgonjwa akichuma thawabu. Mgonjwa anaweza kuchuma thawabu na anaweza asichume thawabu. Asipochuma thawabu atakuwa si mwenye kusafishwa. Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kusema:

إن شاء الله

“Allaah akitaka.”

ni kama matarajio mgonjwa huyu kupata thawabu na hivyo maradhi yake yakawa ni kusafishwa. Katika hali hiyo hakupingani na kufungamanisha du´aa na matakwa.

Miongoni mwa mambo yaliyokatazwa pia ni yale yanayofanywa na baadhi ya watu wanaposema:

اللهم إني لا أسألك رد القضاء ولكني أسألك اللطف فيه

“Ee Allaah! Hakika mimi sikuombi kurudisha makadirio nyuma lakini hata hivyo nakuomba unifanyie upole.”

Haya ni maovu. Bali muombe Allaah akufanyie wepesi, akufanye kutohitajia na muombe Allaah akufunze na wala usiombe kwamba humuombi kurudisha makadirio nyuma. Kwa sababu hakuna kinachorudisha makadirio nyuma isipokuwa tu du´aa. Ni watu wangapi ambao walikuwa wamekurubia kifo ambapo wakaomba du´aa wao au wakaombewa du´aa na Allaah akawaponya. Kilicho muhimu ni kwamba maneno haya hayatakikani kusemwa:

اللهم إني لا أسألك رد القضاء ولكني أسألك اللطف فيه

“Ee Allaah! Hakika mimi sikuombi kurudisha makadirio nyuma lakini hata hivyo nakuomba unifanyie upole.”

Ndugu! Muombe Allaah afya. Usimuombe Allaah akufanyie upole.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1569
  • Imechapishwa: 05/03/2020