Namna ya kumnusuru mwenye kudhulumu na mwenye kudhulumiwa

Swali: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametuamrisha kumnusuru ndugu muislamu ni mamoja amedhulumu au amedhulumiwa. Ni vipi nitamnusuru ndugu yangu mwenye kudhulumu?

Jibu: Kumnusuru kwako ndugu mwenye kudhulumu ni wewe kumzuia kuendelea kufanya hivo. Kumnusuru kwako ndugu mwenye kudhulumiwa ikiwa unaweza kumsaidia ima kwa mkono wako, pesa zako au cheo chako. Kwa sababu kila mmoja kwa kiasi cha uwezo wake. Allaah haikalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadri ya iwezavyo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Swifaat-il-Mu´miniyn https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-09/s_0.mp3
  • Imechapishwa: 22/09/2022