Nadhiri ya kisimamo cha usiku maishani imemshinda

Swali: Mwanamke anasema kuwa alifikwa na tatizo kubwa nyumbani na kuweka nadhiri kwa kusema lau Allaah atanitatulia tatizo langu basi nitasimama usiku na kuswali mpaka pale Allaah ataponifisha. Lakini hata hivyo baada ya muda sikuweza kuendelea na nadhiri yangu. Je, juu yangu kuna kitu kutokana na hili?

Jibu: Ndio, hii ni nadhiri ya wajibu. Kwa kuwa ni nadhiri ya utiifu. Hata hivyo haina maana kuwa asimame usiku mzima. Asimame usiku na kuswali kiasi na atakavyoweza kisha alale. Hii ndio Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa anaswali na kulala. Simama sehemu ya usiku na usisimame usiku mzima. Hili ni lazima kwake katika maisha yake yote. Hata kama atakuwa si muweza aswali angalau kwa kukaa. Swalah jambo lake ni lepesi. Swali angalau kwa kukaa. Na ikiwa hawezi kurukuu na kusujudu ainamishe kichwa. Ikiwa inajuzu kuinamisha kichwa katika swalah za faradhi basi za Sunnah au nadhiri ni aula zaidi. Asiache kusimama usiku. Lakini hata hivyo haina maana ya kwamba asimame usiku mzima. Asimame sehemu ya usiku.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2106
  • Imechapishwa: 01/07/2020