Swali: Ikiwa nadhiri haikuwekewa sharti inakuwa ni yenye kuruhusiwa?

Jibu: Ikiwa ni ya utiifu inamlazimu. Kwa mfano akijilazimisha kufanya kitu fulani kwa ajili ya Allaah ni lazima akifanye. Inahusiana na nadhiri ya utiifu:

”Yeyote atakayeweka nadhiri ya kumtii Allaah basi na amtii.”

Hata hivyo kwa mfano akisema ”Nitafanya – Allaah akitaka”, sio nadhiri. Mfano mwingine akasema ”Nikihudhuria nitafanya”, haimlazimu. Sio nadhiri. Mfano mwingine akasema ”Nitawatolea darsa” au ”Nikimpata fulani nitamnasihi”. Hizo ni ahadi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22892/حكم-النذر-غير-المشروط
  • Imechapishwa: 28/05/2025