Swali: Miongoni mwa ndugu zetu mmoja ametuletea karatasi zilizochapishwa zenye zaidi ya kurasa saba. Ndani yake ameleta utafiti wa kutia shaka mbele ya wanazuoni na watu wa elimu. Anadai kuwa mwisho wa dunia utatokea baada ya miaka 298 na kwamba hilo linapatikana katika mwanzo wa baadhi ya Suurah. Ameleta pia hoja kutoka Qur-aan kuwa dunia itamalizika baada ya miaka 298. Hatujui ametegemea nini katika madai haya. Kijitabu chote kiko mbele yenu, ee Shaykh.
Jibu: Hakika khabari hii tumeisikia siku zilizopita. Maneno haya aliyoyasema mtu huyu ni miongoni mwa ukhurafi na ni ujinga wa hali ya juu. Haifai kabisa kuyazingatia wala kutegemea chochote kutoka humo. Bali ni upotevu ulio wazi. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amebainisha katika Qur-aan Tukufu katika Aayah kadhaa kuwa Qiyaamah hakijui yeyote isipokuwa Yeye tu na hakuna anayejua kitakuja lini isipokuwa Allaah. Aidha amesema pia kuwa Qiyaamah hakitakuja isipokuwa ghafla. Hivyo basi haifai kabisa kuzingatia madai ya aina hii. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anasema:
إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ
”Hakika Allaah ana ujuzi wa Saa.”[1]
Vilevile Akataja mambo mengine manne ya ghaibu.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Funguo za ghaibu ni tano.. .”
Miongoni mwayo ni ujuzi wa Qiyaamah. Hakuna anayejua isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Qur-aan imesema:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي ۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلَّا هُوَ ۚ ثَقُلَتْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً ۗ يَسْأَلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنْهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ اللَّـهِ
”Wanakuuliza kuhusu Saa ni lini kitatokea? Sema: ”Hakika ujuzi wake uko kwa Mola wangu. Hakuna wa kuidhihirisha wakati wake isipokuwa Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitokufikieni isipokuwa kwa ghafla. Wanakuuliza kana kwamba wewe unaijua vyema. Sema: ”Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah.”[2]
Kwa hiyo Allaah pekee ndiye mwenye kuijua, jambo ambalo wanazuoni wote wameafikiana juu yake. Hakuna makinzano baina yao Hakuna anayejua dunia imebakiwa na miaka mingapi. Inaweza kuwa imebaki miaka 2000, 3000 au zaidi au chini, hakuna yeyote anayejua. Ujuzi wa hilo uko kwa Allaah pekee kwa maafikiano ya wanazuoni.
Aayah nyingi za Qur-aan, Hadiyth Swahiyh za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maafikiano ya wanazuoni vyote vinaonyesha wazi kuwa hakuna mwenye kujua Qiyaamah isipokuwa Allaah (Ta´ala).
Kwa hiyo kila jaribio la kutoa tarehe au mwaka wa kutokea Qiyaamah kinyume na Qur-aan na Sunnah ni batili kabisa. Bali ni ukhurafi na ni kusema juu ya Allaah bila elimu. Mtu huyu anatakiwa aelekezwe atubie, na kama hatotubia basi anastahili kuuliwa hali ya kuwa kafiri Kwani anayesema Saa itakuwa siku fulani, mwaka fulani au saa fulani, ni mtu mjinga, mwenye kupotea na ni kufuru. Anatakiwa kuelekezwa kutubia. Vinginevyo ni wajibu kumuua hali ya kuwa kafiri na mwenye kuritadi. Hii ni kwa sababu anamkanusha Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah anasema wazi kuwa hakuna anayeijua Saa isipokuwa Yeye, ilihali yeye anadai kuijua. Hakuna anayesema maneno kama haya isipokuwa mtu aliyepatwa na tatizo katika akili na dini yake.
[1] 31:34
[2] 07:187
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1109/ما-حكم-تحديد-نهاية-العالم-بوقت-معين
- Imechapishwa: 18/08/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1109/ما-حكم-تحديد-نهاية-العالم-بوقت-معين
Imechapishwa: 18/08/2026
https://firqatunnajia.com/mwisho-wa-dunia-ni-mwaka-wa-298/