Inampasa mwalimu ajipambe na tabia njema ambazo Shari´ah imezileta, sifa nzuri na mwenendo unaoridhiwa ambao Allaah amemwelekeza kwazo kama kuipa nyongo dunia, kupunguza kutokana nayo, kutoipa umuhimu pamoja na watu wake, ukarimu na utoaji, tabia njema, kuwa na uso wenye bashasha bila kufikia mpaka wa upuuzi, upole na subira, kujiepusha na mapato duni, kushikamana na uchamungu, unyenyekevu, utulivu, heshima, unyenyekevu, kujishusha, kujiepusha na kucheka na mzaha kupitiliza.

Anatakiwa kudumu katika majukumu yaliyowekwa katika Shari´ah, kama kujisafisha kwa kuondoa uchafu na nywele ambazo Shari´ah imeamrisha ziondolewe, kufupisha masharubu, kukata kucha, kuchana ndevu, kuondoa harufu mbaya na mavazi yanayochukiza.

Ajihadhari tahadhari kubwa kabisa na husuda, kujionyesha, kujiona na kuwadharau wengine, hata kama wako chini yak.

Isitoshe inampasa kutumia Hadiyth zilizokuja kuhusu utajo wa Allaah na du´aa, atambue kuwa Allaah (Ta´ala) anamchunga katika hali yake ya siri na ya dhahiri, adumishe juu ya hayo na iwe tegemeo lake katika mambo yake yote ni kwa Allaah (Ta´ala).

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 28
  • Imechapishwa: 18/08/2026