Mwisho mbaya wa walao nguruwe katika Biblia

14Wakati mtakapoona jambo hili, mioyo yenu itashangilia,

nanyi mtastawi kama majani;

mkono wa Bwana utajulikana kwa watumishi wake,

bali ghadhabu yake kali

itaonyeshwa kwa adui zake.

15Tazama, Bwana anakuja na moto,

magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli,

atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali,

na karipio lake pamoja na miali ya moto.

16Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake

Bwana atekeleza hukumu juu ya watu wote,

nao wengi watakuwa ni wale

waliouawa na Bwana.

17 Watu wote wanaojiweka wakfu na kujitakasa wenyewe ili kwenda bustanini,

wakimfuata aliye katikati ya wale ambao hula nyama za nguruwe na panya pamoja

na vitu vingine vilivyo machukizo, watafikia mwisho wao pamoja, asema Bwana.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Isaya 66:14-17
  • Imechapishwa: 18/01/2020