Mwenye kuwasifu makafiri na Ahl-ul-Bid´ah ni katika wao

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kuwasifu Ahl-ul-Bid´ah ilihali ni mwenye kujua kuwa ni Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal? Je, na yeye anaingia katika Ahl-ul-Bid´ah?

Jibu: Ndio. Anaingia katika wao. Mwenye kuwasifu Ahl-ul-Bid´ah ni katika wao. Mwenye kuonelea kuwa madhehebu yao ni mazuri ni katika wao. Kadhalika mwenye kuwasifu makafiri na yeye pia ni kafiri. Mwenye kusifu ukafiri na akawatetea makafiri na yeye ni kafiri kama wao – na tunaomba kinga kwa Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4745
  • Imechapishwa: 01/05/2015