Swali: [Sauti haiko wazi]
Jibu: Mwenye kuvipinga anapinga Qur-aan. Qur-aan imenukuliwa kwetu kwa mapokezi mengi na pia imenukuliwa na Ummah mzima. Kadhalika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy imenukuliwa na Ummah mzima. Nenda jangwani ambapo kunaishi wasiokuwa waarabu na uulize kuhusu “Swahiyh-ul-Bukhaariy” wanajisalimisha nayo kwa vile ni Imaam al-Bukhaariy. Nenda katika maktabah mbalimbali utakuta maelfu ya nukhsa ya kitabu hichi. Nenda katika maktabah za Misri, Uturuku, India, Palestina na kila utakapo. Hata ukitaka Ulaya na Amerika nenda na utakuta maelfu ya nuskha ya kitabu cha al-Bukhaariy. “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy kuna uwezekano hata mayahudi na manaswara wakawa hawakipingi na badala yake wanajisalimisha nacho. Ni kitabu ambacho kimepokelewa kwa mapokezi mengi na kimeenea kati ya waislamu na wasiokuwa waislamu.
Huyu mwenye kukipinga ni mjinga katika akili zake. Huyu mwenye kusema hivi haiheshimu akili yake.
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=7539
- Imechapishwa: 06/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)